Statoil Heroes of Tomorrow top 10 Announced

Majina kumi ya mwanzo wanao wania kinyang`anyiro cha kumsaka kijana mwenye wazo zuri la kibiashara na hatimae mchanganuo wa biashara Heroes Of Tomorrow Business Competition yametajwa jana na Meneja wa shindano hilo bw. Erick Mchome, kwenye barua ya mwaandishi iliyotolewa na Meneja wa Staitoil nchini Bw. Qystein Michelsen.

Heroes of tomorrow ama Mashujaa wa kesho ni shindano linaloendeshwa na kampuni ya mafuta na gesi kutoka Norway hapa nchini kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi ya Tanzania kwa kutafuta vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 ambao watakuwa na mawazo mazuri ya biashara ili kuwasaidia katika ndoto zao hizo kwa kufanya kuwa kweli.

“Shindano linalenga vijana kutoa mawazo yao ya kibiashara ambayo baadae yatafanywa kuwa biashara” alisema Meneja wa shindano hilo Bw. Mchome.

Shindano hilo limeanza na vijana wa Lindi na Mtwara ambapo vijana 400 walijitokeza kushiriki wakilenga maswala ya kilimo, ufugaji, IT, viwanda vidogodogo na maswala mengine yanayohusiana na biashara ambapo baadhi walijikusanya kama kikundi na wengine mmoja mmoja.

40 bora walichaguliwa kushiriki katika mafunzo ya ujasiliamali yaliyolenga kukuza na kuendeleza biashara ili ziwe na mafanikio ambapo katika hilo kumi bora walichanguliwa.

Walio chagulia kumi bora ni Razaki Kaondo, Nyenje Chikambo, Edward Timamu, Saleh Rashid Kisunga, Azizi Doa, Sifael Nkiliye, Said Selemani, Yunus Mtopa, Yahay Omari, Kastus Kambona na Abdalah Selega. Hata hivyo mchakato bado unaendelea kwani kumi hawa watachuana vikali kwa kuleta michanganua yao ya biashara ambayo itafanyiwa tathmini na baraza la Jury ili kuwapata tano bora na hatimae mshindi.

“Tano bora watatetea michanganuo yao ya biashara mbele ya baraza la Jury” alisema Bw. Mchome ikiwa ni sehemu ya kumtafuta mshindi wa shindano hilo.

Mshindi atapatikana tarehe 15 April jijini Dar es salaam, atazawadiwa dola za kimarekani 5000 wanne walioingia tano bora kila mmoja wao atajipatia dola 1500 na waliofanikiwa kuingia kumi bora kila mmoja wao atapata dola 1000. 

Darecha partners with Mo Dewji Foundation to support start-ups

In a move to recognize and  support young entrepreneurs in Tanzania, the chairman of Mo Dewji Foundation, Forbes Africa Person of the Year and the young billionaire on the continent has partnered with Darecha Limited to provide growth capital, mentorship and networks to high potential start-ups/small businesses.

In order to achieve their mission, Mo Dewji Foundation and Darecha Limited have launched  Mo Entrepreneurs Competition project. Mo Entrepreneurs Competition is a collaborative effort between Mo Dewji Foundation and Darecha Limited to recognize and support the efforts of young entrepreneurs in Tanzania. The competition launches a platform that will enable Mohammed Dewji (The CEO of MeTL Group and Chairman of Mo Dewji Foundation) to support young entrepreneurs who are running highly potential start ups but lack further support in form of growth capital, networks and mentorship  which could accelerate the growth of their start-ups.

In order to participate in this project, download the application form here and Financial Projection Template here. In case you find it difficult to fill the template please call 0656 89 44 69 for further information

Statoil inakukaribisha kushiriki katika shindano la Mashujaa wa kesho


Statoil Heroes of Tomorrow 2015

Tumeshafanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia nchini Tanzania na inasadikika kuwa Tanzania itakuwa kati ya nchi wazalishaji wakubwa wa gesi barani Afrika.Hili linatufanya tuhitaji wajasiriamali wengi wazawa ili kutoa ushirikiano katika sekta hii inayokuwa kwa kasi. Je ungependa kuwa sehemu ya wajasiriamali hao na kutoa mchango wako kwa katika sekta hii kwa kuwa na biashara yako mwenyewe? Shiriki katika shindano letu.

Kuhusu Statoil:

Statoil ni kampuni ya nishati ya kimataifa yenye kufanya shughuli zake katika nchi 36 duniani kote. Statoil ina uzoefu wa miaka 40 katika masuala ya mafuta na gesi na imejikita katika kuwekeza teknolojia ya hali ya juu kuhakikisha kuwa inatoa suluhisho kwa masuala yote ya nishati duniani. Makao makuu ya Statoil yako nchini Norway na kampuni hii inasadikiwa kuwa na wafanyakazi takribani 20,000 duniani kote. Statoil imesajiliwa katika soko la hisa la New York na Oslo.

 

Statoil nchini Tanzania:

Statoil ilianza shughuli zake nchini Tanzania tangu mwaka 2007, iliposaini Mkataba wa Pamoja wa Uzalishaji (PSA) na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa ajili ya Kitalu Namba 2. Statoil Tanzania AS ndio mwendeshaji anaye shiriki kwa kiwango cha 65% cha hisa na ExxonMobil Exploration and Production Limited kwa kiwango cha uwekezaji cha 35%.TPDC ni wawekezaji wa hisa ya asilimia 10% ya leseni endapo kutathibitika kuwepo kiwango cha gesi cha kuwezesha biashara. Statoil na mshirika wake wamefanya ugunduzi mkubwa wa gesi asilia katika kitalu namba 2 eneo linalokadiriwa kuwa na takribani kilomita za mraba 5,500 likiwa kwenye kina cha maji cha urefu wa mita kati ya 1,500 na 3,000. Ugunduzi huu unakadiriwa kuwa 22Tcf (ujazo wa gezi) na hii inapelekea maendeleo makubwa ya mradi wa gesi asilia nchini Tanzania.

 

Statoil inawajali mashujaa wa kesho:

Statoil inaamini katika kuwasaidia vijana wenye vipaji katika nchi ambazo tunafanya shughuli zetu za uchimbaji na uenedelezaji wa nishati. Tunaamaini katika kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao. Kwa njia hii tunaamini tunachangia katika kuendeleza jamii zinazotuzunguka.

Shindano la Mradi wa Biashara:

Shindano la mradi wa biashara la Mashujaa wa kesho lilianzishwa mwaka 2014 ili kuwawezesha vijana mkoani Mtwara kujiajiri kwa njia ya ujasiriamali. Tunawatia moyo vijana kushiriki katika shindano hili la mashujaa wa kesho ili waweze kuzitumia fursa mbalimbali zinazoibuka kutokana na uwepo wa shughuli z asekta ya nishati ya gesi asilia mkoani Mtwara. Shindano hili linalenga mawazo ya biashara ndogo ndogo zinazoweza fanyika mkoani Mtwara. Shindano hili kwa mwaka 2015 lilizinduliwa tarehe 27 Novemba. Shindano litakuwa na awamu mbili; kwanza kutoa wazo la biashara ambapo mwisho wa kukusanya mawazo ya biashara utakuwa ni tarehe 20 Desemba, 2015 saa kumi kamili jioni. Mawazo haya ya biashara yatachujwa na mnamo tarehe 20 Januari 2016 mawazo arobaini ya kwanza yatatajwa na wahusika watafahamishwa ili waweze kuanza kushiriki semina ya mafunzo ya namna ya kuandika mpango wa biashara. Mipango ya biashara itakusanywa tarehe 29 Februari na mnamo tarehe 15 March mipango kumi bora ya biashara itatajwa na washindi watakabidhiwa kwa majaji ili kuweza kupata tano bora na hatimaye kumi bora. Mshindi wa shindano la Mashujaa wa Kesho kwa mwaka 2015 atatangazwa tarehe 14 Aprili, 2016.

 

Vigezo na Masharti ya shindano

 • Washiriki wanaweza shiriki shindano katika vikundi au mtu mmoja mmoja. Kikundi kisizidi watu watatu
 • Washiriki wawe na umri wa 18 – 25 na ni LAZIMA wawe wanaishi Mtwara au Lindi
 • Mshiriki/Kikundi cha washiriki kitaruhusiwa kuwasilisha wazo moja tu la biashara
 • Mshiriki/Washiriki watapaswa kujaza fomu inayopatikana katika kipeperushi hiki
 • Mshiriki/Washiriki wanaweza kushiriki kwa kutumia lugha ya kiingereza au Kiswahili
 • Wazo la biashara lazima lilenge mazingira ya Mtwara na liweze fanyika Mtwara pia.
 • Mshiriki/Washiriki ni lazima walete wazo la biashara au mpango wa biashara walioundaa wenyewe
 • Tarehe ya mwisho kukusanya wazo la biashara itakuwa ni 20 Desemba, 2015
 • Mawazo bora ya biashara yatachaguliwa na washiriki watapewa mafunzo ya namna ya kuandika mpango wa biashara
 • Washiriki wa tano bora watatakiwa kutetea mipango yao ya biashara mbele ya majaji wa shindano hilo.
 • Mshindi atatangazwa tarehe 14 Aprili, 2016
 • Mshindi atapata zawadi ya dola 5000 za kimarekani (Zaidi ya Milioni 10) 
 • Washindi wanne watakaofuata watapata zawadi ya dola 1,500 za kimarekani kila mmoja (au kila kikundi)
 • Mshindi wa shindano atatakiwa kuandika ripoti ya kuonesha jinsi ambavyo fedha alizopata kutoka Statoil zimemsaidia katika kufanya biashara yake. Hili litapaswa kufanyika miezi nane baada ya mshindi kutangazwa.
 • Wafanyakazi wa Statoil wala ndugu zao wa karibu hawataruhusiwa kushiriki shindano hili

Unaweza kutuma wazo lako la kibiashara kwa anuani zifuatazo

 1.  E-Mail: gm_tanzaniahot2014@statoil.com
 2. P.O.Box 713, Dar es Salaa (andika Heros of Tomorrow juu ya bahasha)
 3. Unaweza kuchukua fomu na kuwasilisha wazo lako katika vituo vifuatavyo;
 • Stella Maris University (Mtwara)
 • Naliendele Agricultural Insititute (Mtwara)
 • Chuo cha Utumishi wa Umma (Mtwara)
 • Chuo cha TIA (Mtwara)
 • Chuo cha VETA (Mtwara)
 • Pride FM Radio (Mtwara)
 • Ofisi za Statoil Mtwara Shangani (mbele kidogo ya Maisha Club)
 • Maktaba ya Mkoa wa Mtwara

Unaweza kupata fomu kwenye vituo tajwa hapo juu au kwa ku- BONYEZA HAPA